Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kupitia Mradi wake wa Kituo cha
Mpira wa Miguu kijulikanacho kama NSSF-REAL MADRID Sports Academy
wameanza mchakato wa kusaka vijana wenye vipaji watakao jiunga na kituo
hicho.
Akiongea na waandishi wa Habari Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo
Dr. Ramadhani K. Dau alisema mradi huo ukiwa kama sehemu ya uwekezaji wa
NSSF ulianza maramoja baada ya kusaini mkataba. NSSF imeanza utaratibu
wa kuwabaini vijana walengwa ambapo kwa kuanzia utafutaji wa vipaji vya
mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa
chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji utafanyika kiwilaya kwa Wilaya za
mkoa wa Dar es salaam na utakuwa unafanyika katika viwanja vya Karume.
Uandikishaji
wa washiriki utakuwa unafanyika siku za mwisho wa wiki ili kutoathiri
wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi tarehe 14 , 15, 22 na
23 Februari 2015, na kufuatiwa na michezo ya majaribio tarehe 28
Februari,na Tarehe 1 Machi 2015 kwa wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam
ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume kuanzia saa 1 (moja) asubuhi
hadi saa 9(tisa) alasiri.
Zoezi la Uandikishaji halitahusisha gharama
zozote kwa washiriki, na uandikishaji wa washiriki utafanyika kwa
kujaza fomu maalum na kupewa namba ya ushiriki na kila mshiriki atapata
fursa ya kucheza katika awamu mbili za dakika 30. Kwa kuanzia washiriki
watatakiwa kuja na vifaa vyao vya michezo.
Zoezi la awali litafanywa
na wataalam wa ndani ya nchi ambapo Vijana 500 kati ya wote
watakaofanyiwa majaribio wataingia katika awamu ya pili ya majaribio na
watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu ya Real Madrid na hatimaye
kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia katika shule maalum ya mafunzo
kwa awamu ya kwanza. Wakati wa uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja
na wazazi/walezi wao wakiwa na vitambulisho vyao,na kijana husika awe na
Cheti halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha mbili za
pasipoti rangi ya blue.Muda wa uandikishaji na majaribio unaweza
kuongezwa kulinagana na mahitaji.
Shirika la NSSF linatoa wito kwa
vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo
na kujiajiri katika tasnia hiyo
No comments:
Post a Comment