Katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa furaha,wakazi wa jiji la
Dar es Salaam na vitongoji vyake wataweza kupata burudani za aina
mbalimbali katika tamasha kubwa la Pasaka litakalofanyika katika ufukwe
wa maraha wa Coco beach chini ya maandalizi ya Vodacom Tanzania.
Akiongea
juu ya tamasha hili kubwa ambalo hivi sasa limeanza kuwa gumzo ya
jiji,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema mipango
yote kuhusiana na tamasha hilo imekamilika kinachongojewa ni kuwasha
moto wa burudani kwa wateja wa Vodacom na wananchi wote kwa ujumla.
“Kama
ilivyo kawaida yetu ya kuwapatia huduma bora wateja wetu sambamba na
kuwaburudisha zamu hii tumewaandalia tamasha hili ili waweze kuburudika
katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka ambapo pia watapata fursa ya
kukutana na wasanii mbalimbali wawapendao na kuwa karibu nao ukiwa ni
mwendelezo wa promosheni ya Vodacom ya kuleta burudani kwa wateja
inayojulikana kama Ishi Kistaa”.Alisema.
Nkurlu
alisema kuwa tamasha hilo litakalofanyika siku ya Jumapili ya Pasaka
litaanza asubuhi saa tano kwa burudani mbalimbali za muziki na michezo
kwa ajili ya watoto ambapo baadaye jioni wasanii mbalimbali wa
bongofleva na aina nyingine ya muziki watapanda jukwaani kutoa burudani
kwa washabiki watakaohudhuria kwenye tamasha hilo.
Alisema wako wasanii wengi wamejipanga kutoa kuburudisha wapenzi
wa muziki baadhi yao wakiwa ni Shilole na Bob Junior na wengineo.
“Wateja na mashabiki watapata fursa ya kuonana na mastaa ambao
wanawapenda pia tunawakumbusha wachukie nafasi ya kushiriki katika
promoshe ya Ishi kistaa kwa kutuma neno STAR kwenda 15670”.
Alimalizia
kwa kusema kuwa hali ya amani na usalama inatarajiwa kutawala kwenye
tamasha hili kwa kuwa kuna ulinzi wa kutosha kuhakikisha wananchi
wanapata burudani murua kwa utulivu wakiwa na familia zao na aliahidi
kuwa wateja wa Vodacom na wananchi wengine wanaokaa mbali na Dar es
Salaam wakae mkao wa kula kwa kuwa mikakati inaandaliwa kupeleka
burudani za aina hii katika sehemu mbalimbali nchini kwenye sikukuu
mbalimbali zijazo katika siku za usoni.
No comments:
Post a Comment