Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limekuwa likiendesha Kliniki ya
Huduma kwa Wateja katika viwanja vya TCC Chang'ombe kuanzia Tarehe 20
/03/2015 mpaka Tarehe 29/03/2015 ambapo huduma mbalimbali zimekuwa
zikitolewa.
Huduma hizo ni pamoja na Kutoa Elimu kwa Wanachama na wasio
Wanachama kuhusu mafao yapatikanayo kutoka NSSF, Kutoa Elimu ya miradi
kama Viwanja Vilivyopimwa na Vyenye Huduma za maji, barabara na Umeme
vya kiluvya, Nyumba za Kijichi awamu ya Tatu, Pia wanachama waliweza
kupata Taarifa za michango yao . Uandikishaji wa Wanachama wapya pia
ulifanyika katika Viwanja hivyo.
Akizungumza wakati alipotembelea banda hilo Mgeni Rasmi, Mkurugenzi
Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Prof.
Herman Mwansoko aliisifia Kliniki hiyo ya NSSF kwa kuweza kuwa karibu na
wateja lakini Pia alivutiwa na Teknolojia Mpya ya kuandikisha wateja
kupitia kifaa cha TazPad ambacho kinaweza kuchukua taarifa zote za
wanachama bila kuhitaji uwepo wa Kompyuta.
Kutokana na Umuhimu wa kuwafikia wanachama wetu, Kliniki hiyo
itafanyika Tena siku ya Tarehe 12/04/2015 kwenye Viwanja hivyo vya TCC
Chang'ombe.
No comments:
Post a Comment