Thursday, June 26, 2014

HII NDO HISTORIA YA MAISHA YA MTANGAZAJI MILLARD AYO, KAMA UIKUA HUIJUI KARIBU KUISOMA

Millard Afrael Ayo alizaliwa Arusha January 26 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye famili ya watoto wanne ya Afrael Ayo ambae ni mmeru wa Akheri Tengeru, ni mfanyabiashara na mama Mary Ayo ni mwalimu.

Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Millard, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 12 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 16 mwaka 2002, sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia Patandi Primary School Tengeru, Akeri Secondary School na Mbezi beach high school.

Wakati akisubiri majibu, Millard alijiunga na Arusha College of Electronics na kusomea ufundi wa kutengeneza satelitte dish, tv deck na radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na marafiki zake ili Millard arudishwe shule kuendelea na masomo ya sekondari kitu ambacho alikikubali lakini hakikua na mapokezi mazuri kwa Millard kwa sababu yeye alihitaji kufanya kitu kingine kwa wakati ule.
Mambo yalibadilika pale uncle wake aitwae Gabriel aliekua Marekani aliporudi Tanzania na kumshawishi mama Millard amuache mtoto afanye kile anachotaka na anachokipenda, hapo ndipo Millard akapata nafasi ya kwenda kujiunga na East Africa Training Institute kusomea utangazaji na uandishi wa habari mwaka 2004.

Baada ya mwaka mmoja Millard alijiunga na TVZ Zanzibar kwa muda wa miezi mitano na akarejea Dar es salaam April 2005 kutafuta kazi baada ya hali kuwa ngumu kwenye familia na kukosa pesa kwa ajili ya kujiendeleza na masomo.

Alifanikiwa kupata kazi May 23 2005 kwenye kituo cha Wapo Radio 98.0 ambayo aliambiwa hatolipwa kwa sababu kanisa lililokua linamiliki radio hiyo halina pesa ila kwa sababu alikua na njaa ya maisha na kazi ilibidi aifanye kama ameajiriwa, kazi ilikua jumatatu mpaka jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi huku kazi yake kubwa aliyopangiwa ni kukusanya habari za bei za bidhaa na hali ya usafi kwenye masoko Dar es salaam, pia kwenda kitengo cha MOI Muhimbili hospitali kuchukua habari za majeruhi na vifo vya ajali mbalimbali.

Kutokana na jitihada hizo Millard alianza kulipwa shilingi elfu tano kwa wiki mwezi wa pili baada ya kazi hivyo akawa na mshahara wa elfu 20 kwa mwezi, mshahara ambao uliongezeka na kufikia elfu 20 kwa mwezi kwenye mwaka wa tatu na wa mwisho akiwa Wapo Radio.

Baada ya hapo Millard alijiunga na ITV/Radio One mwaka 2008 ambako alisikika kwenye vipindi mbalimbali lakini MILAZO 101 na habari za michezo ITV ndio vilimpa umaarufu mpaka November 2010 alipojiunga na Clouds FM/TV na kuanza kusikika kwenye kipindi cha AMPLIFAYA december 6 2010 na baadae kukabidhiwa CLOUDS FM Top 20 June 2013.

Mpaka sasa Millard Ayo ni mmiliki wa tuzo 4 ikiwemo ya Mtangazaji bora 2006 kutoka Tanzania Radio Awards, Website bora 2012 kutoka Vodacom Tanzania na African Stars, na moja ni ya heshima akiwa mwandishi pekee kutunukiwa kutoka kwenye familia ya Marehemu mwigizaji Steven Kanumba.

Kipindi cha AMPLIFAYA pamoja na website yake ya millardayo.com ndio vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke.

Kitu ambacho watu wengi hawakifahamu, kipaji cha Millard Ayo kilionekana kwanza na aliyekua mtangazaji wa TBC1 Joseph Msami ambae kwa wakati huo ndio aliona uwezo wa Millard na kumshawishi boss wa Wapo radio kutoa ruhusa ya Millard kuingizwa studio kuwa mtangazaji na sio tena ripota.

Mtu wa pili ambae ndio alizidi kumnyanyua Millard kiutangazaji ni Godwin Gondwe ambae alimuona Millard toka akiwa Wapo Radio, kwanza ndio alikua mtu wa kwanza kumpa Millard dili la kurekodi tangazo la radio la bei kubwa 2007 toka ameanza utangazaji, lilikua la laki moja na nusu za Kitanzania na ndio ilikua pesa kubwa Millard kuwahi kulipwa kwa kazi ya mikono yake toka azaliwe, na ni pesa kubwa kuliko hata mshahara wake kwa mwezi wakati huo ambao ulikua shilingi elfu sitini.

Shukrani za pekee kwa Reginald Mengi, Joyce Muhavile, Julius Nyaisanga, Deogratius Rweyunga, Abdallah Mwaipaya na Isack Gamba ambao walikua kama wazazi/marafiki wakati Millard akiwa ITV, pamoja na kwamba kwa sasa hayupo ITV lakini urafiki wao haujaisha na Millard amekua balozi wao mzuri

No comments:

Post a Comment