Mwanamke mmoja ameamua kujitokeza
hadharani na kusema kuwa katika maisha yake tayari amekwishatembea na
wanaume elfu 10 asilimia 90 wakiwa wameoa katika harakati zake za
kujitafutia kipato.Gwyneth Montenegro alikulia nchini Australia katika
shule binafsi kabla ya kwenda kuwa mmoja wa wasichana makahaba
wanaolipwa pesa nyingi zaidi akipata zaidi ya dola 2,000 kwa usiku mmoja
kutoka kwa wateja wake.
Anafafanua
zaidi sababu za kujiingiza kwenye biashara hiyo moja ikiwa ni
kutokujiamini na kutaniwa sana alipokuwa shule kutokana na kuwa na aibu
sana hivyo kupelekea wanafunzi wenzie kumchokoza.
Wakati wengi wa marafiki zake waliishia
kuwa madaktari na wengine wanasheria, Gwyneth aliingia katika biashara
hiyo na kufanikiwa kulala na wanaume 10,091 na kuweka taarifa za
kumbukumbu ya kila mmoja wao.
Wateja wake wengi walikuwa ni wazungu
wenye pesa zao na ingawa asilimia 90 ni waume za watu, Gwyneth anasema
hajutii kwani kwa kufanya hivyo inawezekana ameokoa ndoa zao kwa kiasi
kikubwa.
No comments:
Post a Comment