Staa wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amefunguka kuwa anaamini
amepigwa ‘juju’ kutokana na kuugua ugonjwa ambao haukutambulika
hospitalini.
Akizungumza machache na paparazi wa GPL akiwa nyumbani kwake
anapougulia maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bozi alisema,
anaamini amerogwa na wasanii wenzake wasiopenda maendeleo baada ya
kupata dili la kucheza filamu katika Kundi la Kaole.
“Roho inaniuma sana yaani ni jinsi gani wasanii tulivyokuwa
hatupendani, ghafla tu nilipofika nyumbani baada ya kutokea Moro kwenye
dili la kazi hali yangu ilibadilika, nikahisi kichwa kuniuma sana na
maumivu makali tumboni, nilipoenda hospitali niliambiwa sina tatizo
ikanilazimu nitafute mtaalamu na kuyabaini hayo maana lengo lao walitaka
kunimaliza, nashukuru Mungu kwa sasa nimepata nafuu,” alisema Bozi.
No comments:
Post a Comment