Hii ya leo inahusu tukio lililotokea huko Florida Marekani,
ambapo mtoto mwenye umri wa miaka 13, amemshambulia kaka yake mwenye
umri wa miaka 16 pamoja na mdogo wake mwenye umri wa miaka 6, kwa
kuwapiga na risasi halafu akajipiga mwenyewe.
Polisi wamesema watoto hao walikuwa peke
yao nyumbani kwao wakati mama yao akiwa kazini wakaanza kugombania
chakula, mtoto huyo akachukua bastola na kuanza kuwashambulia wenzake,
kaka yake alipiga simu Polisi ambao walifika eneo la tukio na
kumkimbiza Hospitali lakini mtoto aliyewapiga risasi pamoja na mdogo
wake walikutwa wameshafariki.
Polisi wanafanya uchunguzi kujua jinsi mtoto huyo alivyoweza kupata silaha hiyo.
No comments:
Post a Comment