Diamond Platnumz ni msanii mwengine mkubwa wa Kitanzania
aliyejiunga na Mkito.com kwaajili ya kusambaza muziki wake mtandaoni. Msanii
huyu anajiunga na wengine kama Fid Q, Nay Wamitego, Rich Mavoko, Vanessa Mdee,
Juma Nature, Barnaba, Linah, Belle 9 na wengine wengi katika mchakato
unaoendelea kuwawezesha wasanii kujipatia kipato kutokana na muziki wao
kupakuliwa kwenye mtandao.
Diamond kabla ya kuondoka kuelekea Afrika ya Kusini kwaajili
ya video yake mpya aliona ni vyema kuungana na Mkito.com kwani ni kampuni ya
Kitanzania yenye madhumuni mazuri kwa tasnia ya muziki nchini.
Watumiaji wote wa Mkito.com sasa wanaweza kupata nyimbo za
Diamond kupitia www.mkito.com ikiwemo albam ya Best Of Diamond na pia wimbo
wake mpya Mdogomdogo.
No comments:
Post a Comment