Tuesday, June 10, 2014

SOMA ALICHOSEMA PROF J BAADA YA DIAMOND KUKOSA TUZO

Msanii mkongwe wa Hip Hop Proffesor Jay amesema kuwa kushindwa kwa Diamond kuchukuwa tuzo za MTV kusimvunje moyo kwakuwa alikuwa anashindana na wasanii wakubwa sana Africa.

Akizungumza na mtandao huu leo ,Proffesor Jay amesema kuwa nafasi aliyopata Diamond na kushindana na wasanii hayo ni ushindi mkubwa wake.
“Diamond lazima ajue katika mashindano kuna kushinda na kushindwa, Kitu ambacho ninaweza kumwambia Diamond asikate tamaa, ameshindanishwa na wasanii wakubwa sana ambao pia ni advantage kwake ,msanii kama Davido pamoja na kufanya muziki mzuri tutambue kuwa nyuma yake kuna Wanageria zaidi ya milioni 150, ambao kiukweli wenzetu wameamka sana kuchangia kuwa support wasanii wao, sisi Watanzania tumekuwa tunazungumza kwa maneno mengi kulipo vitendo ,so mtu kama Davido ameshinda kwa kupigiwa kura na watu wake wengi na muziki wake umefika afrika nzima. Kwaiyo kushindwa kwake Diamond asichukulie kukata tamaa ,yeye achukulie kama changamoto na kuwashawishi Watanzania na mashabiki wake kuendelea ku support muziki wake ili afike mbali zaidi, naamini kuna kila dalili kwa Diamond kuendelea kufanya vizuri zaidi hapo mbeleni, pia nataka niwaambie 

No comments:

Post a Comment