Monday, June 9, 2014
ALIKIBA SASA KUWASAHAULISHA MACHUNGU WABONGO, HII NIBAADA YA DIAMOND KUKOSA TUZO MTV MAMA,
Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba hivi karibuni wanatarajiwa
kuwasahaulisha wabongo na story zote za mtv mama, na kuhusu yote
yaliyojiri kwa kuwaletea bonge la show litakalofanyika pale new maisha
club jumapili hii.Huu ni ujio mpya wa Alikiba baada ya kukaa kimya kwa
muda mrefu bila kuonekana hata kwenye media mbali mbali za hapa bongo,
jambo lilowafanya baadhi ya fans wa Alikiba na muziki wa bongo fleva kwa
ujumla, kujiuliza kama mkali huyu amepotezea muziki au la. Habari
zilizo chini ya kapeti zinasema kuwa kiba yuko chimbo sasa hivi
akijipanga kwa ujio wake mpya kabisa, na sasa hivi anapasha tu kwa
makubwa aliyoandaa kipindi chote alichopotea kwa muda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment