Meneja wa Muigizaji maarufu wa Bongo
Movie Wema sepetu amewaacha midomo wazi watu waliokuwa wamehudhuria Tuzo
ya Muziki ya Kilimanjaro katika ukumbi wa mlimani City jana baada ya
kupaniki na kujikuta anajibu mapigo kwa Mc wa sherehe hiyo Silvery Mjuni
anayefahamika zaidi kwa jina la Mpoki.
Meneja wa Wema aitwae Martin Kadinda
amejikuta ameshindwa kuzuia hisia zake kutokana na masihara ya mpoki
pale alipowaambia kuwa timu Diamond ni kikundi kinachoongoza kupost
picha hata zisizo na msingi kwenye mitandao ya kijamii hususani
Instagram,
Mpoki aliwaambia Diamond na wafuasi
wake akiwemo Wema, Martin Kadinda,Rommy Johnson kuwa wanapost kila
wakati kwa mfano wakiwa wanakula, wamelala ndipo Martin Kadinda
alipomwambia Mpoki kuwa atafute namna nyingine ya kutafutia pesa
Kauli ya Kadinda iliwashangaza wengi
kwani licha ya kuwa Mpoki alikuwa anazungumza kimasihara lakini jambo
lake lina ukweli kwa kiasi kikubwa japo Kadinda alikuwa mwepesi kupaniki
na kushindwa kukubaliana na ukweli huo...
No comments:
Post a Comment